Vijana wa Muleba Wako Uso kwa Uso na Waziri wa Maendeleo ya Vijana
Vijana kutoka Wilaya ya Muleba walipata fursa ya kukutana uso kwa uso na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nanauka, wakati wa ziara yake ya kikazi katika mkoa huo.
Katika mkutano huo, vijana walieleza changamoto wanazokabiliana nazo katika shughuli zao za kiuchumi, wajasiriamali na maendeleo ya kijamii. Waziri Nanauka aliwasikiliza kwa makini na kutoa mwongozo pamoja na ushauri kuhusu jinsi ya kutumia fursa za serikali na miradi ya uwezeshaji wa vijana.
Vilevile, aliwahimiza vijana kushirikiana, kubuni miradi yenye tija na kutumia ipasavyo mikopo na programu zinazotolewa na Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana ili kuongeza kipato na kuimarisha maendeleo ya jamii zao.
- "Huduma bora: Mafunzo ya NeST Morogoro yaiweka Ofisi ya...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Nanauka, ak...
- Makundi maalumu ikiwemo Vijana waaswa kujiunga NeST kupata fursa ya 30% ya Zab...
- Huduma bora kwa watanzania, NeST kutoa fursa kwa wazabuni wa...
Serikali imekabidhi pikipiki 22 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 87 kw...