Ofisi ya Rais
Maendeleo ya Vijana
Maadili ya Msingi

Maadili ya Msingi

 

 

  1. Uzalendo na Umoja wa Kitaifa: Kukuza upendo kwa nchi, amani, utulivu na uraia wenye kuwajibika miongoni mwa vijana.
  2. Ujumuishi na Usawa: Kuhakikisha kuwa vijana wote, wakiwemo wanawake vijana, vijana wenye ulemavu na wale wanaoishi katika maeneo ya vijijini na yaliyotengwa, wananufaika na afua za maendeleo.
  3. Uwajibikaji na Uadilifu: Kudumisha uwazi, maadili mema ya utendaji na usimamizi unaolenga matokeo.
  4. Ushirikiano na Ubia: Kufanya kazi kwa pamoja na serikali, sekta binafsi na jamii ili kuongeza athari chanya ya programu na mipango ya maendeleo.