Ofisi ya Rais
Maendeleo ya Vijana
WAZIRI NANAUKA: KILA SIKU NI FURSA YA KUJENGA UWEZ...

WAZIRI NANAUKA: KILA SIKU NI FURSA YA KUJENGA UWEZO WAKO

16 Jul, 2026
WAZIRI NANAUKA: KILA SIKU NI FURSA YA KUJENGA UWEZO WAKO

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Nanauka, akizungumza na vijana katika hafla ya kukabidhi vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya udereva iliyofanyika Makambako, Mkoani Njombe, leo Julai 15, 2026.

Katika hotuba yake, Mhe. Nanauka amewahimiza vijana kujenga mazoea ya kujifunza kila siku kwa kuongeza ujuzi na uzoefu katika fani wanazozifanya, akieleza kuwa kujifunza kwa vitendo na kuendelea kujiendeleza kitaaluma ni msingi wa kuongeza ushindani, kupata ajira na kufanikiwa katika shughuli za kiuchumi.