- "Huduma bora: Mafunzo ya NeST Morogoro yaiweka Ofisi ya Rais - Maendeleo ya Vijana kwenye viwango vipya vya uwazi."
- "Kasi mpya, kidijitali zaidi: Maafisa Ofisi ya Rais - Maendeleo ya Vijana 'waiva' kwenye mfumo wa NeST, tayari kuwatumikia!"
KATIKA hatua ya mapinduzi makubwa ya kiutendaji na utoaji huduma, Ofisi ya Rais - Maendeleo ya Vijana imehitimisha mafunzo ya Mfumo wa Taifa wa Ununuzi wa Umma kielektroniki (NeST) kwa maafisa wake. Hatua hii sio tu ni ushindi kwa serikali katika kurahisisha utendaji, bali ni habari njema na ufunguo wa fursa mpya kwa vijana kote nchini.
Mafunzo hayo yamehitimishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bi. Edith Semtengu akimwakilisha Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, amesema Serikali imelenga kuwanoa maafisa ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya kidijitali. Lakini, kwa kijana mjasiriamali, fundi, au yule aliye kwenye kikundi anajiuliza; "Je, kuhitimu kwa maafisa hawa kunamsaidia vipi?"
_1784309722.jpg)
“Mfumo wa NeST umeundwa mahususi kuleta uwazi, haki na usawa. Kwa kuijengea uwezo timu ya maafisa kutoka Ofisi ya Rais - Maendeleo ya Vijana, jambo ambalo litaenda kuongeza Ushiriki Huru kwenye Zabuni za Serikali, Kasi ya Utekelezaji wa Miradi ya Vijana, Thamani Halisi ya Fedha na Kuchochea Ukuaji wa Kampuni za Vijana, ameyasema hayo Bi. Semtengu.
Sanjari na hayo, Mkufunzi kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Bw. Wilson Samwel, amesema ni matarajio ya umma wa watanzania kushuhudia Huduma Bora kutokana na Mafunzo ya NeST ambayo yanaenda kuiweka Ofisi ya Rais - Maendeleo ya Vijana Kwenye Viwango Vipya vya Uwazi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Nanauka, ak...
- Makundi maalumu ikiwemo Vijana waaswa kujiunga NeST kupata fursa ya 30% ya Zab...
- Huduma bora kwa watanzania, NeST kutoa fursa kwa wazabuni wa...
Serikali imekabidhi pikipiki 22 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 87 kw...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Nanauka, am...