Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nanauka amesema Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Vijana itaendelea kuimarisha uratibu wa elimu ya uraia na uzalendo ili kuongeza ari ya vijana kupenda taifa na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya Taifa.
Amesema kuwa, hatua hiyo itahusisha uratibu wa majukwaa ya vijana katika ngazi ya mikoa na halmashauri, pamoja na kuimarisha utoaji wa elimu ya uraia na uzalendo katika Halmashauri 184 nchini.
Vilevile, Mhe. Nanauka amesema kwamba Wizara itaendelea kuratibu mbio za Mwenge wa Uhuru na maadhimisho ya wiki ya vijana kitaifa, hatua inayolenga kukuza mshikamano, uzalendo na uwajibikaji miongoni mwa vijana.
Kadhalika, amesema Serikali itasimamia maadhimisho ya siku ya wanaojitolea kimataifa, siku ya vijana Afrika na siku ya vijana kimataifa, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha ushiriki wa vijana katika shughuli za maendeleo ndani na nje ya nchi.
Aidha, amesisitiza kuwa juhudi hizo zinalenga kujenga kizazi cha vijana chenye maadili, uzalendo na utayari wa kushiriki katika shughuli za kijamii, kisiasa na kiuchumi za kuliendeleza taifa.
- "Huduma bora: Mafunzo ya NeST Morogoro yaiweka Ofisi ya...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Nanauka, ak...
- Makundi maalumu ikiwemo Vijana waaswa kujiunga NeST kupata fursa ya 30% ya Zab...
- Huduma bora kwa watanzania, NeST kutoa fursa kwa wazabuni wa...
Serikali imekabidhi pikipiki 22 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 87 kw...