Ofisi ya Rais
Maendeleo ya Vijana
WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA AVUTIWA NA BANDA LA...

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA AVUTIWA NA BANDA LA OFISI YA RAIS – MAENDELEO YA VIJANA KATIKA MAONESHO YA 50 YA SABASABA

01 Jul, 2026
WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA AVUTIWA NA BANDA LA OFISI YA RAIS – MAENDELEO YA VIJANA KATIKA MAONESHO YA 50 YA SABASABA

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga, ametembelea Banda la Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), ambapo amejionea huduma mbalimbali zinazotolewa na Ofisi hiyo pamoja na maonesho ya bidhaa kutoka kwa wajasiriamali waliowezeshwa kupitia programu za Serikali.

Katika ziara hiyo, Mhe. Kapinga amepatiwa maelezo kuhusu huduma zinazotolewa katika banda hilo, zikiwemo Elimu ya masuala ya sheria, Elimu ya uzalendo, huduma za Mfumo wa Youth Empowerment System (YES) pamoja na fursa mbalimbali zinazoratibiwa na Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana kwa ajili ya kuwawezesha wananchi, hususan vijana.

Mhe. Kapinga amepongeza juhudi zinazofanywa na Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana katika kusogeza huduma karibu na wananchi kupitia maonesho hayo. Pia amewapongeza wajasiriamali waliowezeshwa na Serikali kwa ubunifu wao na matumizi mazuri ya fursa walizopata, huku akihimiza wananchi kuendelea kutembelea banda hilo ili kupata elimu na huduma mbalimbali zinazotolewa.