WAZIRI NANAUKA AWEKA MIKAKATI YA KUWAWEZESHA VIJANA NA WANAWAKE KIUCHUMI
Serikali kupitia Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuwawezesha vijana na wanawake kiuchumi kupitia program za uwezeshaji zinazotekelezwa na Wizara za kisekta kwa kutoa mafunzo ya ujuzi wa ujasiriamali, ubunifu na matumizi ya teknolojia kulingana na mahitaji ya soko la ajira.
Akizungumza Bungeni jijini Dodoma Mei 29, 2026 , Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Nanauka amesema Serikali imejipanga kuhakikisha vijana, wanawake makundi mengine yanapata mazingira bora yatakayowawezesha kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji na maendeleo ya Taifa.
Mhe. Nanauka amesema pamoja na juhudi zinazofanyika kwa vijana kupitia Tsh.Bilioni 200 iliyolewa, Serikali imeendelea kuwawezesha wanawake kupitia mikopo inayowasaidia kukuza biashara zao na kuongeza kipato cha familia.
Mhe. Nanauka ameongeza kuwa Wanawake wanaendelea kunufaika kupitia mifuko na program za wizara za kisekta, pamoja na mfuko wa Maendeleo ya Vijana ambapo wanawake 147 wa Mkoa wa Arusha wanatarajia kunufaika na mkopo huo Mwanzoni mwa Mwezi Juni mwaka 2026 , fedha zitakazowasaidia kuendesha shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwemo biashara ndogo ndogo, uzalishaji pamoja na huduma zinazochangia maendeleo ya jamii.
Aidha, Serikali inaendelea kushirikiana na Sekta Binafsi ikiwemo Taasisi za Benki, Mashirika yasiyo ya Serikali kwa kutoa Elimu kabla ya Mikopo, wakati wa Mikopo na baada ya kupatiwa Mikopo ili kutambua umuhimu wa matumizi sahihi ya mikopo hiyo ili iwe chachu ya maendeleo endelevu kwa wananchi.
Serikali imeendelea kuahidi kuimarisha programu za uwezeshaji ili kuhakikisha wananchi wengi zaidi, hususan vijana na wanawake, wanafikiwa na fursa za maendeleo Nchini.
- "Huduma bora: Mafunzo ya NeST Morogoro yaiweka Ofisi ya...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Nanauka, ak...
- Makundi maalumu ikiwemo Vijana waaswa kujiunga NeST kupata fursa ya 30% ya Zab...
- Huduma bora kwa watanzania, NeST kutoa fursa kwa wazabuni wa...
Serikali imekabidhi pikipiki 22 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 87 kw...