Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Nanauka amewataka watumishi wa Wizara hiyo kuongeza uwajibikaji, weledi na ubunifu katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuharakisha maendeleo ya vijana nchini.
Mhe. Nanauka ameyasema hayo leo Mei 22, 2026 katika ukumbi wa Mikutano wa Dodoma Jiji-Mtumba wakati akizungumza na watumishi wa Wizara hiyo katika kikao kilicholenga kujadili kuhusu utendaji kazi wa watumishi na muelekeo wa Wizara.
Akizungumza na watumishi wa Wizara hiyo, Mhe. Nanauka amesema watumishi wa Wizara ya Maendeleo ya Vijana wamepewa fursa ya kipekee ya kuandika historia ya kuanzisha na kuweka Misingi imara ya utendaji kazi utakaoleta matokeo chanya kwa vijana na Taifa kwa ujumla.
“Tumepata nafasi ya kuitumikia Serikali katika kipindi cha kihistoria cha kuanzishwa kwa Wizara hii. Hii ni fursa ya kukua, kujifunza mambo mapya, kuzoea utaratibu mpya wa kazi na kujenga familia mpya ya kikazi yenye lengo moja la kuwahudumia vijana,” amesema Mhe. Nanauka.
Aidha, amesisitiza kila mtumishi anatakiwa kuonesha uwezo wa kujiongoza na kujituma badala ya kusubiri maelekezo akisisitiza kuzingatia dhana ya Ubora katika kila jambo wanalofanya kwa kuhakikisha matokeo yanayozalishwa yanakidhi viwango vya juu vya utendaji.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana Bi. Jenifa Omolo amesema dhamira yao ni kuhakikisha Wizara inawahudumia vijana kwa kasi, ubora na ufanisi mkubwa, huku kila mtumishi akitambua kuwa kila jambo analofanya linaacha alama katika historia na mafanikio ya Wizara hiyo.
_1779465811.jpeg)
Akizungumza kwa niaba ya watumishi, Mkurugenzi wa Idara ya Malezi na Maongozi kwa Vijana, Godfrey Massawe amemshukuru Waziri Nanauka kwa nasaha kwa watumishi na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo yaliyotolewa ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa bidii ili kutimiza malengo yaliyowekwa na Wizara hiyo.
- "Huduma bora: Mafunzo ya NeST Morogoro yaiweka Ofisi ya...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Nanauka, ak...
- Makundi maalumu ikiwemo Vijana waaswa kujiunga NeST kupata fursa ya 30% ya Zab...
- Huduma bora kwa watanzania, NeST kutoa fursa kwa wazabuni wa...
Serikali imekabidhi pikipiki 22 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 87 kw...