Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, leo Julai 5, 2026, amewasili katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam, kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Fainali za Vijana Uchumi Challenge 2026.

Mara baada ya kuwasili ukumbini, Mhe. Dkt. Nchemba ametembelea na kukagua mabanda mbalimbali ya taasisi za Serikali na wadau wa maendeleo, akipata maelezo kuhusu huduma na bunifu zinazowasilishwa. Ziara hiyo imeonesha dhamira ya Serikali ya kuendelea kuunga mkono ubunifu, ujasiriamali na jitihada za maendeleo ya uchumi kupitia ushiriki wa vijana na taasisi mbalimbali.

Fainali za Vijana Uchumi Challenge 2026 zimewakutanisha washiriki, viongozi wa Serikali, sekta binafsi na wadau wa maendeleo kwa lengo la kuhamasisha ubunifu na kutambua mchango wa vijana katika kukuza uchumi wa Taifa.
- "Huduma bora: Mafunzo ya NeST Morogoro yaiweka Ofisi ya...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Nanauka, ak...
- Makundi maalumu ikiwemo Vijana waaswa kujiunga NeST kupata fursa ya 30% ya Zab...
- Huduma bora kwa watanzania, NeST kutoa fursa kwa wazabuni wa...
Serikali imekabidhi pikipiki 22 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 87 kw...