Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Jakaya Kikwete, amefungua rasmi Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma leo tarehe 16, Juni 2026 katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma. Maadhimisho hayo yanahusisha wizara, taasisi na mashirika mbalimbali ya umma yanayotoa huduma kwa wananchi.
Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, Waziri Kikwete amesisitiza umuhimu wa watumishi wa umma kuendelea kutoa huduma kwa weledi, uwajibikaji na uadilifu ili kuimarisha imani ya wananchi kwa Serikali. Pia amehimiza matumizi ya teknolojia za kidijitali katika kuboresha utoaji wa huduma na kuongeza ufanisi wa utendaji kazi serikalini.
Maonesho hayo yanatoa fursa kwa wananchi kupata elimu, ushauri na huduma mbalimbali kutoka kwa taasisi za umma katika eneo moja. Washiriki wa maonesho wanatumia jukwaa hilo kuonesha mafanikio, ubunifu na maboresho yaliyofanyika katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
Wananchi wa Dodoma na maeneo ya jirani wamehamasishwa kutembelea maonesho hayo ili kujifunza zaidi kuhusu huduma zinazotolewa na Serikali pamoja na kutoa maoni yatakayosaidia kuendelea kuboresha utumishi wa umma nchini. Maadhimisho hayo yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 23,Juni 2026 katika Viwanja vya Chinangali Park.
- "Huduma bora: Mafunzo ya NeST Morogoro yaiweka Ofisi ya...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Nanauka, ak...
- Makundi maalumu ikiwemo Vijana waaswa kujiunga NeST kupata fursa ya 30% ya Zab...
- Huduma bora kwa watanzania, NeST kutoa fursa kwa wazabuni wa...
Serikali imekabidhi pikipiki 22 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 87 kw...