Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana Mhe. Joel Arthur Nanauka, amefanya Mkutano na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Kituo cha Urithi na Ukombozi wa Afrika, kutambulisha shindano la kitaifa la vijana linalolenga kuwapa vijana nafasi ya kutoa mawazo yao ya kiubunifu, yatakayoleta suluhu ya changamoto zinazoikabili Tanzania.
Shindano hilo lililopewa jina la ‘Vijana Uchumi Challenge” likiwa na kauli mbiu Wana Wanafikiri, Taifa Linasonga, ni hatua za makusudi za kuwezesha Tanzania kukabiliana, kustahimili na kuendana na mabadiliko ya kisiasa, kiuchumi na kijamii yanayojitokeza duniani kwasababu ya migogoro ya kimataifa, ushindani mkubwa wa kiuchumi, na kasi ya mabadiliko ya teknolojia.
Mhe. Nanauka amesema kwamba shindano hilo ni la umuhimu mkubwa kwani litasaidia kuibua vijana wenye uwezo mkubwa wa ubunifu, fikra mpya na mtazamo mpya kuhusu dunia inayobadilika, na hivyo kuiweka Tanzania katika nafasi nzuri ya kustahimili misukosuko ya kimataifa.
“Vijana Uchumi Challenge inalenga kutumia kikamilifu rasilimali vijana ambao ni nguvu kazi kubwa ya taifa letu, ili kuimarisha uzalishaji wa ndani, kuwekeza katika ubunifu na teknolojia, pamoja na kuhamasisha wananchi wote kushiriki kikamilifu katika kutafuta suluhisho la changamoto za kiuchumi zinazoikabili nchi yetu.”
Utambulisho wa shindano hilo la “Vijana Uchumi Challenge” umeenda sambamba na utambulisho wa Kamati ya Kitaifa ya Vijana itakayoratibu na kusimamia shindano hilo. Aidha, Mhe. Nanauka amewataka vijana wote wa Tanzania kuwa tayari kukamata fursa ya Vijana Uchumi Challenge ili kuleta fikra chanya za kuliendeleza taifa kuelekea Dira ya Taifa, 2050.
- "Huduma bora: Mafunzo ya NeST Morogoro yaiweka Ofisi ya...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Nanauka, ak...
- Makundi maalumu ikiwemo Vijana waaswa kujiunga NeST kupata fursa ya 30% ya Zab...
- Huduma bora kwa watanzania, NeST kutoa fursa kwa wazabuni wa...
Serikali imekabidhi pikipiki 22 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 87 kw...