Ofisi ya Rais
Maendeleo ya Vijana
VIJANA PLATFORM TEMEKE MWENDO MDUNDO

VIJANA PLATFORM TEMEKE MWENDO MDUNDO

12 Apr, 2026
VIJANA PLATFORM TEMEKE MWENDO MDUNDO

-Vijana waapa kudumisha uzalendo,Kuulinda Mwenge 
-Waziri Nanauka azidi kung'ara kwa maono
-Temeke yafunika kwa mahudhurio ya Vijana 

Na Byarugaba Innocent, DSM 

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe.Sixtus Mapunda leo Aprili 12,2026 ameongoza Kongamano la Vijana sambamba na Uzinduzi wa Vijana platform hafla iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Shule ya Sekondari Kibasila ukihudhuriwa na zaidi ya Vijana 360 kutoka maeneo mbalimbali ya kata za Wilaya ya Temeke.

Pamoja na mambo mengine Vijana wameaswa  kufufua Moyo wa kujitolea na Uzalendo katika jamii na kujenga Taifa lenye lenye watu wanaoishi kwa amani, umoja, upendo pamoja na kuheshimu utawala wa Sheria, kuwa waadilifu na kuishi katika utamaduni wa uwajibikaji.

Aidha,Vijana wamefunzwa elimu ya uraia kwa lengo la kujenga mshikamano na umoja wa kitaifa huku wakitakiwa Kuulinda Muungano wetu kwa wivu mkubwa.

Joseph Eliaman Mgugu amesema yeye kama kijana kongamano la Vijana limekuwa baraka na  fursa kwani limekuja kutatua changamo zinazowakumba Vijana wengi hapa Tanzania hasa kwenye suala uzalendo na kudumisha umoja na mshikamano.

Aidha, Waziri Nanauka ameelezewa kuwa Kiongozi wa mfano kwa Vijana wengi kwani mafunzo anayotoa kupitia mitandao ya Kijamii limeendelea kuwa suluhisho la matatizo ya Vijana hasa kwenye sekta za elimu, uchumi, uongozi na siasa kwa kuwa mung'amuzi wa woga na kujenga uthubutu na matumizi sahihi ya fursa zilizopo ndani na nje ya Tanzania.

Kwa upande wake Najma Nuru Ally Mwanafunzi wa kidato cha tano shule ya Sekondari Kibasila amesema kongamano limemfungulia Dunia kwani amekuwa mjuvi wa mambo mengi kupitia mada zilizotolewa hasa za uzalendo na uraia.

Anna Rumishasia Maricca afisa Maendeleo ya Vijana Manispaa ya Temeke ameipongeza Wizara ya Maendeleo ya Vijana kwa kubuni na kutekeleza  Ptaform za Vijana kwani zinasaidia kuwaibua na kuwaunganisha na vijana ili kujenga umoja na mshikamano wa Kitaifa, kuleta Maendeleo ya Taifa pamoja na kuwaunganisha na fursa zinazolewa na serikali na wadau wa Maendeleo 

Ameongeza kuwa platform hizi  ziwe endelevu kwa lengo la kusikikiza maono, changamoto,kupokea hoja na ushauri kutoka kwa Vijana na kuzitafutia ufumbuzi ili ziwafanye Vijana kushiriki kwenye kujenga uchumi endelevu wa Taifa


Kongamano hili linakwenda sambamba na kaulimbiu mbiu isemayo Vijana tuyajenge, Tanzania ni yetu linatelezwa Aprili 12 -13,2026 kuelekea Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru Aprili 14,2026.