Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mheshimiwa Joel Arthur Nanauka, ametembelea Kiwanda cha Missenyi Standard Chalks, ambacho ni kiwanda cha vijana kilichopo Wilaya ya Missenyi, Kata ya Mutukula.
Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Waziri alikagua shughuli za uzalishaji na kujionea maendeleo ya kiwanda hicho kinachoendeshwa na vijana, ambacho ni miongoni mwa wanufaika wa mkopo wa asilimia kumi (10%) ya Halmashauri. Mradi huo umewezesha vijana kuongeza uzalishaji, kuunda ajira na kuchangia ukuaji wa uchumi wa eneo hilo.
Mheshimiwa Nanauka alipongeza juhudi za vijana hao na kusisitiza kuwa Serikali itaendelea kuwekeza katika kuwawezesha vijana kiuchumi kupitia mikopo na fursa mbalimbali, ili kukuza ujasiriamali na maendeleo endelevu ya taifa.
- "Huduma bora: Mafunzo ya NeST Morogoro yaiweka Ofisi ya...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Nanauka, ak...
- Makundi maalumu ikiwemo Vijana waaswa kujiunga NeST kupata fursa ya 30% ya Zab...
- Huduma bora kwa watanzania, NeST kutoa fursa kwa wazabuni wa...
Serikali imekabidhi pikipiki 22 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 87 kw...