Serikali kupitia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Mhe. Prof. Riziki Shemdoe imehimiza matumizi ya mifumo ya TEHAMA ili kuongeza ufanisi wa taasisi za Serikali katika kutoa huduma kwa wananchi.
Akihutubia mamia ya watumishi katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma leo Juni 23, 2026, viwanja vya Chinangali Park, Dodoma, Mhe. Shemdoe ameelekeza Mamlaka ya Serikali Mtandao, Tanzania (eGA) kuendelea kushirikiana na taasisi za umma kuboresha na kuanzisha mifumo itakayoongeza ufanisi wa utendaji kazi wa taasisi za umma.

Akimwakilisha Katibu Mkuu Kiongozi amepongeza ushiriki wa taasisi za umma katika maonyesho hayo, na kuelekeza Maafisa Utumishi wote nchini kuwajibika ipasavyo na kwa weledi ili kuepukana na malalamiko ya upandishwaji madaraja haswa watumishi wa umma wanaostahili na kutimiza vigezo vya msingi.

Aidha Mhe. Shemdoe ametumia fursa hiyo kuipongeza Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, ikiwa ni miongoni mwa taasisi 226 za serikali zilizoshiriki kikamilifu maadhimisho hayo kuanzia Juni 16, 2026 na kufika kilele leo, yakiwa kaulimbiu isemayo, “Kuchochea uwajibikaji jumuishi kwa huduma endelevu.”
- "Huduma bora: Mafunzo ya NeST Morogoro yaiweka Ofisi ya...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Nanauka, ak...
- Makundi maalumu ikiwemo Vijana waaswa kujiunga NeST kupata fursa ya 30% ya Zab...
- Huduma bora kwa watanzania, NeST kutoa fursa kwa wazabuni wa...
Serikali imekabidhi pikipiki 22 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 87 kw...