Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nanauka amesema kuwa Serikali imejipanga kikamilifu kuimarisha Uratibu na Ushirikishaji wa Vijana katika Masuala ya Kijamii, Kiuchumi na Kisiasa.
Hayo yamesemwa leo Aprili 20, 2026 bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha mpango na makadirio ya bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2026/2027.
Mhe. Nanauka amebainisha kuwa hatua hizo zinalenga kuimarisha ushiriki wa vijana katika maendeleo ya taifa, kwa kuzingatia kuwa zaidi ya asilimia 55 ya nguvu kazi ya taifa inatokana na kundi hilo.
Amesema kuwa, pamoja na kuimarisha uratibu na ushirikishaji wa vijana kupitia maandalizi ya Mfumo wa Taifa wa kuratibu masuala ya vijana pia itaanzishwa kanzidata ya kitaifa itakayosaidia kukusanya na kuchambua taarifa muhimu za maendeleo ya vijana nchini ili kuwezesha ufanisi wa programu hizo.
Katika hatua nyingine, vijana watawezeshwa kushiriki katika majukwaa ya kikanda, eneo la Maziwa Makuu na kimataifa, sambamba na kukusanya maoni yao kupitia dawati la huduma kwa wateja ili kuboresha utekelezaji wa programu mbalimbali za maendeleo.
Aidha, Serikali itafanya mapitio ya Sheria ya Baraza la Vijana la Taifa Sura ya 441 na kuandaa Mkakati wa Kitaifa wa Vijana, Amani na Usalama, hatua inayolenga kuongeza ushiriki wa vijana katika masuala ya amani na usalama ndani na nje ya nchi.
Pia Wizara itasimamia utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007, toleo la 2024, ili kukuza ajira, ujasiriamali na ujuzi kwa vijana pamoja na kuimarisha ushiriki wao katika maamuzi na uongozi.
- "Huduma bora: Mafunzo ya NeST Morogoro yaiweka Ofisi ya...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Nanauka, ak...
- Makundi maalumu ikiwemo Vijana waaswa kujiunga NeST kupata fursa ya 30% ya Zab...
- Huduma bora kwa watanzania, NeST kutoa fursa kwa wazabuni wa...
Serikali imekabidhi pikipiki 22 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 87 kw...