Ofisi ya Rais
Maendeleo ya Vijana
OFISI YA RAIS - MAENDELEO YA VIJANA YASHIRIKI MAFU...

OFISI YA RAIS - MAENDELEO YA VIJANA YASHIRIKI MAFUNZO YA VIJANA WAZABUNI NA MAKUNDI MAALUM MJINI SONGEA

18 Jun, 2026
OFISI YA RAIS - MAENDELEO YA VIJANA YASHIRIKI MAFUNZO YA VIJANA WAZABUNI NA MAKUNDI MAALUM MJINI SONGEA

Ofisi ya Rais - Maendeleo ya Vijana (OR - MV) imeshiriki mafunzo ya kuwajengea uwezo vijana wazabuni na makundi maalum yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA), yaliyofanyika tarehe 18 Juni, 2026 katika Ukumbi wa Manispaa ya Songea Mjini, Mkoa wa Ruvuma.

Akifungua mafunzo hayo, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa – Mipango na Uratibu, Bw. Jumanne Makoo, alimewahimiza vijana na makundi maalum kuchangamkia fursa za kiuchumi zinazotolewa na Serikali ili kujikwamua kiuchumi, kuongeza kipato na kuchangia maendeleo ya Taifa.

Vilevile, ameipongeza PPAA kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana katika kutoa elimu na kuhamasisha vijana na makundi maalum kunufaika na fursa hizo.

Kwa upande wa Ofisi ya Rais - Maendeleo ya Vijana, mada imewasilishwa na Bw. Rashid Luhuiy, ambaye ameainisha fursa mbalimbali za uwezeshaji wa kiuchumi zinazoratibiwa na Ofisi hiyo na kuwahimiza vijana kuzitumia ipasavyo kwa kuwekeza katika ubunifu, nidhamu, uadilifu na uwajibikaji.

Pia, amewahamasisha kutumia kikamilifu fursa ya asilimia 30 ya zabuni za umma inayotengwa kwa ajili ya vijana na makundi maalum kwa mujibu wa sheria na kanuni za ununuzi wa Umma, akisisitiza kuwa uzingatiaji wa sheria, taratibu na maadili ya kazi ni msingi muhimu wa mafanikio na ushiriki wao katika maendeleo ya Taifa.