Nanauka Azindua Jukwaa la Vijana, Awahimiza Kushiriki Kikamilifu katika Maendeleo ya Taifa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nanauka amezindua rasmi Jukwaa la Vijana (Vijana Platform) linalolenga kuwakutanisha vijana ili kujadili masuala ya maendeleo, ubunifu na fursa mbalimbali za kiuchumi.
Uzinduzi wa jukwaa hilo umefanyika kwa ushiriki wa vijana kutoka maeneo mbalimbali jijini Dar es salaam tarehe 10/01/2026 ambapo limeanzishwa kwa lengo la kutoa nafasi kwa vijana kushirikiana, kubadilishana mawazo na kuibua suluhisho la changamoto zinazowakabili katika nyanja za elimu, ajira na ujasiriamali.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mhe. Nanauka alieleza kuwa jukwaa hilo ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuhakikisha vijana wanapata nafasi ya kushiriki kikamilifu katika michakato ya maendeleo ya taifa la Tanzania.
Alisisitiza kuwa vijana wana nafasi kubwa katika kujenga uchumi wa taifa na kuhimiza washiriki kutumia jukwaa hilo kuibua mawazo bunifu, kujenga mitandao ya ushirikiano na kushiriki katika miradi ya maendeleo itakayosaidia kujitegemea kiuchumi.
Aidha, alibainisha kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha vijana wanapata mazingira bora ya kuendeleza vipaji, ubunifu na fursa za kiuchumi.
Kwa upande wao, vijana walioshiriki katika uzinduzi huo walieleza kufurahishwa na kuanzishwa kwa jukwaa hilo wakisema litakuwa fursa muhimu ya kujadili changamoto zao, kubadilishana uzoefu na kupata maarifa yatakayowasaidia kujiendeleza na kuchangia maendeleo ya jamii.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nana...
UN CAREERS LIVESTREAM EVENT 2026 Kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Wahitimu Wapy...
WAZIRI NANAUKA AWEKA MIKAKATI YA KUWAWEZESHA VIJANA NA WANAWAKE KIUCHUMI Seri...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Nanauka ame...
Ofisi ya Rais - Maendeleo ya Vijana kwa kushirikiana na Restless Development leo...