Ofisi ya Rais
Maendeleo ya Vijana
NANAUKA KUJA NA BARAZA LA TAIFA LA VIJANA SHIRIKI...

NANAUKA KUJA NA BARAZA LA TAIFA LA VIJANA SHIRIKISHI

18 Jun, 2026
NANAUKA KUJA NA BARAZA LA TAIFA LA VIJANA  SHIRIKISHI

Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana Julai 13,2026 imeendelea na uratibu wa kukusanya maoni kwa wadau ili kuunda Baraza  la Vijana la Taifaambalo ni  Shirikishi ambapo awamu hii wawakikishi kutoka kwenye  jumuiya za umoja wa Vijana za vyama vya Siasa nchini wameshiriki kuwasilisha maoni yao.

Kaimu Mkurugenzi wa huduma za sheria kutoka Ofisi ya Rais Maendeleo Vijana Bi.Tunu Temu amesema Sheria ya Baraza la Taifa la Vijana Sura 441 ilitungwa kwa lengo la kuweka mfumo rasmi wa ushiriki wa Vijana katika Masuala ya Maendeleo ya Taifa, ambapo kupitia Sheria hii,serikali ilianzisha chombo cha kuratibu Masuala ya Vijana Kuanzia ngazi ya chini hadi Taifa.Hata hivyo,kutokana na mabadiliko ya Kijamii, Kiuchumi na kiteknolojia  kumekuwa  na haja ya kuiboresha sheria hiyo ili kuendana na Mahitaji ya Vijana wa Sasa.

Temu ameongeza kuwa Sheria hiyo inaainisha muundo wa Baraza la Vijana Kuanzia ngazi ya Kata,Wilaya,Mkoa hadi Taifa pamoja na majukumu yake Katika kuhamasisha ushiriki wa Vijana kutoa maoni,ushauri kwa Serikali, kukuza mshikamamo na uzalendo.Hata hivyo pamoja na uwepo wake, utekelezaji wake umeonesha changamoto katika uwakilishi, uratibu na ufanisi kiutendaji 

Temu amefafanua kuwa kutokana na uzoefu na utekelezaji wake, imebainika kuwa kuna haja ya kufanya maboresho ili kuhakikisha Baraza linakuwa jumuishi,lenye kuakisi maslahi mapana ya Vijana nchini ambapo maboresho haya yanakusudiwa kuondoa mapungufu ya ki-muundo,kuongeza ufanisi na utekelezaji wa majukumu ya Baraza.

Joseph Igembe kutoka chama cha (AFP) amempongeza Mhe.Joel Arthur Nanauka,Waziri mwenye dhamana ya Maendeleo ya Vijana kwa kutambua Umuhimu wa uwepo wa Baraza la Vijana la Taifa na kuamua kuweka utaratibu Shirikishi wa kutoa maoni ya kuboresha Sheria na kuundwa kwa Baraza Shirikishi kwa maslahi ya Taifa.

Kwa upande wake Ruqayya Mahmoud Nassiri (CHADEMA) amesema huu ni Mwanzo Mzuri kwa Wizara kushirikisha wadau ili kupokea maoni  yanayopelekea kuundwa kwa Baraza la Vijana ambalo ni Shirikishi 

Masoud Mambo (CHAUMA) amesema yeye kama mjumbe kutoka Chama cha ukombozi wa Umma na wadau wengine wa vyama vya Siasa wamepokea kwa furaha kushirikishwa kwenye mchakato wa kuanza kutengeneza Baraza la Vijana la Taifa kupitia maoni yao.