Waziri Nanauka Akutana na Kikundi cha Youth Connect Kujadili Mawazo Chanya ya Ujenzi wa Taifa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nanauka amekutana na kikundi cha vijana cha Youth Connect katika mazungumzo yaliyolenga kujadili masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya vijana na mchango wao katika kujenga taifa.
Mkutano huo umefanyika jijini Dar es Salaam ambapo pande zote mbili zilipata fursa ya kubadilishana mawazo kuhusu namna ya kuhamasisha vijana kuwa wabunifu, wazalendo na washiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Nanauka alisisitiza umuhimu wa vijana kuwa na fikra chanya, ubunifu na mshikamano ili kuweza kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya Tanzania. Alieleza kuwa Serikali inaendelea kuweka mazingira rafiki kwa vijana ili waweze kutumia vipaji, elimu na ubunifu wao katika kuanzisha miradi ya maendeleo na kujiajiri.
Kwa upande wao, wawakilishi wa kikundi cha Youth Connect walieleza dhamira yao ya kuendelea kuhamasisha vijana kushiriki katika mijadala ya maendeleo, kuibua mawazo mapya na kushirikiana na Serikali katika kuendeleza programu mbalimbali zinazolenga kuwajengea vijana uwezo wa kujitegemea.
Mazungumzo hayo yalisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali na makundi ya vijana katika kuibua na kutekeleza mawazo bunifu yatakayosaidia kujenga jamii yenye maendeleo, mshikamano na matumaini kwa kizazi cha sasa na kijacho.
- "Huduma bora: Mafunzo ya NeST Morogoro yaiweka Ofisi ya...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Nanauka, ak...
- Makundi maalumu ikiwemo Vijana waaswa kujiunga NeST kupata fursa ya 30% ya Zab...
- Huduma bora kwa watanzania, NeST kutoa fursa kwa wazabuni wa...
Serikali imekabidhi pikipiki 22 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 87 kw...