Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nanauka, amewagusa na kuwapa matumaini vijana wenye ulemavu wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la Vijana (Vijana Platform) lililofanyika katika Mkoa wa Mtwara.
Katika tukio hilo, Mhe. Nanauka alisisitiza umuhimu wa kuhakikisha kuwa vijana wote, wakiwemo vijana wenye ulemavu, wanapata fursa sawa za kushiriki katika shughuli za maendeleo, elimu, ujasiriamali na ajira. Alieleza kuwa Serikali inaendelea kuweka mikakati na mazingira rafiki yatakayowawezesha vijana wenye ulemavu kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa.
Aidha, Waziri Nanauka aliwahimiza vijana hao kujiamini, kutumia vipaji na ujuzi walionao pamoja na kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali kupitia programu za uwezeshaji wa vijana.
Kwa upande wao, vijana wenye ulemavu walieleza kufurahishwa na hatua ya Serikali ya kuwajumuisha katika majukwaa ya vijana, wakisema kuwa jukwaa hilo limewapa nafasi ya kusikilizwa, kueleza changamoto zao na kushiriki katika kupanga mikakati ya maendeleo yao.
- "Huduma bora: Mafunzo ya NeST Morogoro yaiweka Ofisi ya...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Nanauka, ak...
- Makundi maalumu ikiwemo Vijana waaswa kujiunga NeST kupata fursa ya 30% ya Zab...
- Huduma bora kwa watanzania, NeST kutoa fursa kwa wazabuni wa...
Serikali imekabidhi pikipiki 22 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 87 kw...