Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nanauka, leo Juni 2, 2026, amekutana na kufanya mazungumzo na ugeni kutoka Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) ulioongozwa na Mkuu wa Taasisi hiyo, Prof. Philipo Sanga, katika ofisi za Wizara zilizopo Mtumba, jijini Dodoma.
Mazungumzo hayo yalijikita katika kuimarisha ushirikiano kati ya Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima katika kubuni na kutekeleza programu zitakazowawezesha vijana kupata elimu, maarifa na stadi mbalimbali za maisha na kazi.
Mhe. Nanauka alieleza kuwa Serikali inaendelea kuweka mkazo katika kuwawezesha vijana kupitia elimu, mafunzo ya ujuzi na teknolojia ili kuongeza ushiriki wao katika shughuli za kiuchumi na maendeleo ya taifa. Aidha, alisisitiza umuhimu wa taasisi za elimu kushirikiana na Serikali katika kuandaa vijana wenye uwezo wa kukabiliana na changamoto za soko la ajira la sasa na la baadaye.
Kwa upande wake, Prof. Sanga aliwasilisha maeneo mbalimbali ya ushirikiano ambayo Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima imekuwa ikiyatekeleza katika kuwawezesha vijana na makundi mengine ya jamii kupitia elimu ya watu wazima, mafunzo ya ufundi na programu za kujifunza kwa kutumia teknolojia za kisasa.
_1780418833.jpeg)
Kikao hicho kimefungua fursa za kuimarisha ushirikiano wa kimkakati kati ya pande hizo mbili kwa lengo la kuongeza fursa za elimu, ujuzi na uwezeshaji wa kiuchumi kwa vijana nchini.
UN CAREERS LIVESTREAM EVENT 2026 Kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Wahitimu Wapy...
WAZIRI NANAUKA AWEKA MIKAKATI YA KUWAWEZESHA VIJANA NA WANAWAKE KIUCHUMI Seri...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Nanauka ame...
Ofisi ya Rais - Maendeleo ya Vijana kwa kushirikiana na Restless Development leo...
KATIKA kuimarisha afya na utendaji kazi mahali pa kazi, Wizara ya Nchi, Ofisi ya...