Ofisi ya Rais
Maendeleo ya Vijana
MAANDALIZI GRAND FINALE VIJANA UCHUMI CHALLENGE Y...

MAANDALIZI GRAND FINALE VIJANA UCHUMI CHALLENGE YAFIKIA PATAMU

19 Jun, 2026
MAANDALIZI GRAND FINALE VIJANA UCHUMI CHALLENGE  YAFIKIA PATAMU

-Mshindi kuzoa Milioni 50

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Vijana Dkt.Kedmon Elisha Mapana leo Juni 19,2026 ameongoza kikao cha awali cha tathmini  ya maandalizi ya fainali ya shindano la Vijana lijulikanalo kama Vijana Uchumi Challenge lililoanza kushindaniwa Mwezi Aprili, 2026 kwa kuwashirikisha Vijana wote nchini.

Shindano hili liliwataka Vijana kuja na ufumbuzi wa mambo ya Kiuchumi,Kijamii yanayotokana na hali halisi ya msuguano wa kivita Mashariki ya Kati na madhara yanayoikabili Dunia kwa sasa ikiwemo kupanda kwa nishati ya Mafuta inayopelekea kupanda kwa bidhaa tumizi katika Maisha ya mwananchi wa kawaida.

Shindano hilo lenye kaulimbiu isemayo "Wanatunafikiri,Taifa linasonga" liliwashirikisha Vijana wa Kitanzania kuja na mawazo chanya ya kulikwamua Taifa kwa changamoto hizo na kulinda kuporomoka kwa Uchumi wa Taifa.

Akitoa taarifa ya Maandalizi, Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya shindano hilo Joseph Malekela amesema maandalizi yamefikia asilimia 90 na kwamba asilimia 10 zilizosalia sitakamilika ndani ya siku mbili kabla ya tarehe 27 Juni,2026 siku ya fainali.

Aidha,amewakaribisha Watanzania wote kuhudhuria hafla hiyo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC) kushuhudia mnyukano wa vijana Kimawazo wakiwasilisha mawazo bunifu mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan anayetarajiwa kuwa Mgeni rasmi.

Kwa upande wake Dkt.Mapana ameipongeza Kamati ya Kitaifa kwa Kazi nzuri ya uratibu na maandalizi wa shughuli inayokwenda kuweka historia kwa Watanzania kujivua fikra pevu za Vijana wao zinapokuwa suluhisho la utatuzi wa changamoto za Kitaifa na Kimataifa