Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2026, Wazo Michael Mwang'onda, amemkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo,Mheshimiwa Ngollo Malenya, kitabu maalum cha kumbukumbu ya Miaka 60 ya Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa ajili ya kutumika kama rejea ya historia, falsafa na mchango wa Mwenge wa Uhuru katika Taifa.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Ndugu Mwang’onda amesema Serikali itaendelea kusimamia na kulinda historia ya Mwenge wa Uhuru kwa kuwa ni alama muhimu ya umoja, uzalendo, maendeleo na mshikamano wa Watanzania.
Amesisitiza kuwa ni wajibu wa viongozi na jamii kwa ujumla kuhakikisha falsafa ya Mwenge wa Uhuru inaendelea kudumishwa na kurithishwa kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
“Kupitia kitabu hiki cha Miaka 60 ya Mbio za Mwenge wa Uhuru, vijana na wananchi wataendelea kujifunza historia ya Taifa letu, misingi ya uzalendo pamoja na mchango mkubwa wa Mwenge wa Uhuru katika kuhamasisha maendeleo ya wananchi,” amesema Mwang’onda.
Kwa upande wake, Suleiman Mvunye, Mkurugenzi wa Idara ya Elimu ya Uraia, Uzalendo na Uratibu wa Mwenge wa Uhuru kutoka Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo Jenifa Omolo, amewataka Wakuu wa Wilaya pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kuendelea kuanzisha na kuimarisha programu mbalimbali za vijana kupitia majukwaa ya Vijana Platform.

Amesema Serikali inalenga kuwafikia vijana, kuwasikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili kupitia mifumo rasmi ya ushiriki wa vijana katika maendeleo ya Taifa.
Aidha, amesisitiza kuwa elimu ya uraia na uzalendo ni nyenzo muhimu katika kujenga kizazi chenye maadili, uwajibikaji na uzalendo kwa Taifa lao.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Mhe. Malenya, ameishukuru Wizara ya Maendeleo ya Vijana kwa kuandaa kitabu hicho cha historia ya Mwenge wa Uhuru akieleza kuwa kitakuwa nyenzo muhimu ya kujifunzia kwa vijana na watoto kuhusu historia, falsafa na mchango wa Mwenge wa Uhuru nchini.
Amesema Wilaya ya Namtumbo itaendelea kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha vijana wanapata elimu sahihi ya uzalendo na kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya Taifa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nana...
UN CAREERS LIVESTREAM EVENT 2026 Kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Wahitimu Wapy...
WAZIRI NANAUKA AWEKA MIKAKATI YA KUWAWEZESHA VIJANA NA WANAWAKE KIUCHUMI Seri...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Nanauka ame...
Ofisi ya Rais - Maendeleo ya Vijana kwa kushirikiana na Restless Development leo...