Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Bi. Jenifa Christian Omolo, leo Juni 13, 2026, amezindua rasmi programu ya kuwawezesha vijana kiuchumi yenye Kauli mbiu isemayo JIKONEKTI KIBIASHARA, iliyoanzishwa na taasisi inayojihusisha na masuala ya maendeleo ya vijana, Youth Connect.
Uzinduzi wa programu hiyo umefanyika katika Ukumbi wa Five Star Hall, Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam, ukihusisha vijana takribani 480, wadau wa maendeleo na wajasiriamali kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Bi. Omolo amesema kuwa programu ya JIKONEKTI KIBIASHARA ni hatua muhimu katika kuwawezesha vijana kupata maarifa,matumizi sahihi ya mitandao na fursa za kiuchumi zitakazowawezesha kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya taifa.
Aidha, Bi. Omolo amempongeza Mkurugenzi na mwanzilishi wa programu hiyo, Bi. Catherine John kwa maono, ubunifu na jitihada zake za kuandaa jukwaa hilo muhimu linalolenga kuwaunganisha vijana na fursa mbalimbali za biashara na ujasiriamali ndani na nje ya nchi.

Amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wanaotekeleza mipango chanya yenye lengo la kuwajengea vijana uwezo wa kujiajiri, kuajiriwa na kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi.
Bi.Omolo amevipongeza vikundi vyote vya Wajasiliamali vilivyoonesha bidhaa zao kwa kuwa na uthubutu wa kuzalisha bidhaa na kutoa rai ya kuwa na matumizi sahihi ya fedha sanjali na kuongeza ubunifu ili kuzalisha bidhaa zinazoweza kushindana kwenye soko la ndani na nje ya nchi.
- "Huduma bora: Mafunzo ya NeST Morogoro yaiweka Ofisi ya...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Nanauka, ak...
- Makundi maalumu ikiwemo Vijana waaswa kujiunga NeST kupata fursa ya 30% ya Zab...
- Huduma bora kwa watanzania, NeST kutoa fursa kwa wazabuni wa...
Serikali imekabidhi pikipiki 22 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 87 kw...