Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Bi. Jenifa Christian Omolo, leo Juni 15,2026 amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa CRDB Bank Foundation ulioongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Bi. Tully Esther Mwambapa.
Mazungumzo hayo yamelenga kujadili maeneo ya ushirikiano kwenye hafla ya utoaji wa tuzo na zawadi kwa washindi wa shindano la Vijana Uchumi Challenge litakalofanyika Juni 27,2026 kwenye Ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Center (JNICC) Kuanzia saa 1 asubuhi likitarajiwa kuwa na wahudhuriaji zaidi ya 3000 kutoka kwenye mikoa yote Tanzania
Pamoja na mambo mengine,Shindano hilo linalenga kuibua na kuhamasisha ubunifu, ujasiriamali na ushiriki wa vijana katika shughuli za maendeleo ya uchumi.
Katika kikao hicho, pande zote mbili zimejadiliana namna bora ya kuhakikisha hafla hiyo inafanyika kwa mafanikio makubwa na kufikia malengo yaliyokusudiwa ya kuwahamasisha vijana kuendelea kubuni na kutekeleza mawazo yenye tija kwa maendeleo yao na ya Taifa kwa ujumla ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan.
- "Huduma bora: Mafunzo ya NeST Morogoro yaiweka Ofisi ya...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Nanauka, ak...
- Makundi maalumu ikiwemo Vijana waaswa kujiunga NeST kupata fursa ya 30% ya Zab...
- Huduma bora kwa watanzania, NeST kutoa fursa kwa wazabuni wa...
Serikali imekabidhi pikipiki 22 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 87 kw...