Mamlaka ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imetembelea Banda la Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) na kutoa elimu kwa vijana wajasiriamali kuhusu umuhimu wa kurasimisha biashara zao.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa BRELA, Theresa Chilambo, amesema wamevutiwa na ubunifu wa vijana wanaoshiriki maoneshoni, lakini akasisitiza kuwa bado wapo ambao hawajasajili biashara zao, jambo linaloweza kuwanyima fursa ya kukuza biashara hadi kuwa kampuni.
Ameongeza kuwa BRELA ina jukumu la kusajili na kurasimisha biashara, kutoa leseni pamoja na kulinda majina ya biashara na chapa (brandi), hatua inayowasaidia wajasiriamali kulinda ubunifu wao dhidi ya matumizi yasiyo halali.
Bi. Chilambo aliongeza kuwa biashara isiposajiliwa inaweza kuchukuliwa na mtu mwingine akaisajili, hali inayoweza kumfanya mmiliki halisi kupoteza haki ya kuitambulisha rasmi.
- "Huduma bora: Mafunzo ya NeST Morogoro yaiweka Ofisi ya...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Nanauka, ak...
- Makundi maalumu ikiwemo Vijana waaswa kujiunga NeST kupata fursa ya 30% ya Zab...
- Huduma bora kwa watanzania, NeST kutoa fursa kwa wazabuni wa...
Serikali imekabidhi pikipiki 22 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 87 kw...