Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Nanauka, amewasili Mkoani Arusha na kupokelewa na viongozi mbalimbali tayari kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Programu ya Mikopo ya Shilingi Bilioni 200 kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, unaotarajiwa kufanyika Julai 9, 2026.

Mara baada ya kuwasili, Mhe. Nanauka ametembelea na kujionea shughuli za wanufaika wa mikopo hiyo ambapo amekutana na wajasiriamali vijana hasa Mama lishe na Baba Lishe wanaonufaika na programu hiyo inayolenga kukuza uchumi, kuongeza ajira na kuwawezesha vijana kujitegemea kupitia biashara na miradi yenye tija .
Ikumbukwe kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan, alitoa Shilingi Bilioni 200 kwa ajili ya kuanzishwa kwa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, unaolenga kuongeza fursa za mitaji nafuu kwa vijana nchini, kuimarisha ujasiriamali na kuchochea ukuaji wa uchumi unaoongozwa na vijana.
_1783541659.jpeg)
Uzinduzi wa programu hiyo unatarajiwa kuwa hatua muhimu katika utekelezaji wa dhamira ya Serikali ya kuwawezesha vijana kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya Taifa.
- "Huduma bora: Mafunzo ya NeST Morogoro yaiweka Ofisi ya...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Nanauka, ak...
- Makundi maalumu ikiwemo Vijana waaswa kujiunga NeST kupata fursa ya 30% ya Zab...
- Huduma bora kwa watanzania, NeST kutoa fursa kwa wazabuni wa...
Serikali imekabidhi pikipiki 22 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 87 kw...