Wataalamu kutoka Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, wizara za kisekta, sekta binafsi na asasi za kiraia wameanza kuandaa andiko dhana la uanzishwaji wa Programu ya Huduma ya Msaada wa Kisaikolojia na Afya ya Akili kwa Vijana, katika siku ya pili ya kikao cha siku tatu kilichofunguliwa jana na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Dkt. Kedmon Mapana, katika Hoteli ya Kibo Peak, mkoani Morogoro.

Kikao hicho kinawaleta pamoja wadau kutoka sekta mbalimbali ili kuchangia mawazo na utaalamu katika kuandaa andiko litakaloweka msingi wa programu ya kitaifa itakayoboresha upatikanaji wa huduma za msaada wa kisaikolojia na afya ya akili kwa vijana.
Programu hiyo inatarajiwa kuimarisha uratibu na ushirikiano kati ya taasisi za Serikali na wadau mbalimbali katika utoaji wa huduma za afya ya akili kwa vijana, ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuimarisha ustawi, ulinzi na maendeleo jumuishi ya vijana nchini.
- "Huduma bora: Mafunzo ya NeST Morogoro yaiweka Ofisi ya...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Nanauka, ak...
- Makundi maalumu ikiwemo Vijana waaswa kujiunga NeST kupata fursa ya 30% ya Zab...
- Huduma bora kwa watanzania, NeST kutoa fursa kwa wazabuni wa...
Serikali imekabidhi pikipiki 22 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 87 kw...