Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana Mhe.Joel Arthur Nanauka leo Oktoba 10,2026 amefika rasmi Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa kuungana na Watanzania wengine kwenye Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, Kumbukizi ya Baba wa Taifa Mwl.Julius Kambarage Nyerere pamoja na maadhimisho ya Wiki ya Vijana,2026
Mhe.Nanauka ametua uwanja wa ndege wa Rukwa na kupokelewa na Mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe.Charles Makongoro Nyerere pamoja na Maafisa wengine waandamizi wa Chama cha Mapinduzi na Serikali.
Aidha,Mhe.Nanauka amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Rukwa,Kamati ya usalama Mkoa kwa maandalizi mazuri kuelekea kuhitimisha Mbio za Mwenge wa Uhuru,2026 ambao mpaka kufikia kilele umekimbia kwenye Mikoa yote 31 yenye Halmashauri 195 za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa,2026 yameanza Oktoba 8 na yanatarajiwa kufunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Oktoba 10,2026
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nana...
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imeitaka Ofisi ya Rais...
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imepongeza maandalizi...
WAZIRI MKUU wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba...
-Asifu bunifu za Vijana zinazozalisha ajira -Atoa ahadi ya kuongeza bajeti ya V...