Ofisi ya Rais
Maendeleo ya Vijana
NANAUKA AKUTANA NA WATENGENEZA MAUDHUI NA WADAU WA...

NANAUKA AKUTANA NA WATENGENEZA MAUDHUI NA WADAU WA TASNIA YA FILAMU, KUJADILI FURSA NA CHANGAMOTO

25 Oct, 2026
NANAUKA AKUTANA NA WATENGENEZA MAUDHUI NA WADAU WA TASNIA YA FILAMU, KUJADILI FURSA NA CHANGAMOTO

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nanauka, amekutana na watengeneza maudhui mtandaoni, watengeneza filamu, waigizaji na wadau wengine wa tasnia ya filamu katika kikao kilichofanyika Protea Hotel Courtyard, kwa lengo la kujadili fursa, changamoto na namna ya kuimarisha maendeleo ya sekta ya ubunifu nchini.

Katika kikao hicho, Mhe. Nanauka amesisitiza umuhimu wa vijana kutumia vipaji, ubunifu na majukwaa yao ya kidijitali kutoa elimu kwa jamii, kuhamasisha mabadiliko chanya na kuchangia maendeleo ya vijana. Aidha, ameeleza umuhimu wa wadau hao kufahamu na kutumia fursa zinazotolewa na Serikali kupitia mifumo mbalimbali ili kukuza shughuli zao na kujiletea maendeleo ya kiuchumi.

Kwa upande wao, wadau hao wamewasilisha changamoto zinazowakabili katika utekelezaji wa shughuli zao, zikiwemo upatikanaji wa mapato kupitia majukwaa ya kidijitali, masuala ya kodi, upatikanaji wa mikopo na fursa za ajira. Pia, wamejadili umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati yao na Serikali katika kutafuta suluhisho la changamoto hizo, kuboresha mazingira ya kazi na kuweka mikakati ya kukuza tasnia ya ubunifu nchini.