Waziri wa Kazi, Ajira, Vijana na Uwezeshaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Ali Suleiman Ameir, amewataka vijana nchini kutumia maarifa na uzoefu walioupata kupitia Kongamano la Vijana la Kitaifa, kutatua changamoto zinazowazunguka, kuanzisha miradi ya uzalishaji mali na kushiriki kikamilifu katika kuleta maendeleo ya taifa.
Ameir ameyasema hayo wakati wa kufunga kongamano hilo lililofanyika Oktoba 11–12, 2026, Manispaa ya Sumbawanga, Mkoa wa Rukwa, akisisitiza kuwa mafanikio ya kongamano hilo yatapimwa kwa namna maarifa yaliyopatikana yatakavyobadilishwa kuwa vitendo na mipango inayozalisha matokeo chanya kwa vijana na jamii.

“Mafanikio ya kongamano hili yatapimwa kwa namna maarifa tuliyopata yanavyobadilika kuwa vitendo, mawasiliano yanavyounganishwa kuwa mipango na mipango hiyo kuleta matokeo chanya katika maisha ya vijana na jamii kwa ujumla,” amesema Ameir.
Amewataka vijana kutumia fursa za kiuchumi zilizopo katika sekta za kilimo, biashara, viwanda na uchumi wa kidijitali badala ya kutegemea ajira za Serikali pekee. Pia, amezitaka taasisi za elimu na mafunzo kuhakikisha ujuzi wanaoutoa unaendana na mahitaji ya soko la ajira na kuwawezesha vijana kujiajiri na kuongeza uzalishaji.

Akizungumzia kaulimbiu ya kongamano hilo, “Mazingira Tofauti, Fursa Sawa kwa Vijana,” Ameir amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha vijana wote wanapata fursa sawa za kuendeleza vipaji na uwezo wao. Aidha, amewataka vijana kudumisha uzalendo, uadilifu, nidhamu na uwajibikaji, huku akizitaka taasisi na wadau wa maendeleo kufuatilia utekelezaji wa maazimio ya kongamano hilo kwa manufaa ya vijana na taifa kwa ujumla.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nana...
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imeitaka Ofisi ya Rais...
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imepongeza maandalizi...
WAZIRI MKUU wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba...
-Asifu bunifu za Vijana zinazozalisha ajira -Atoa ahadi ya kuongeza bajeti ya V...