Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nanauka, amefanya kikao na wadau wa sekta ya mawasiliano kujadili namna ya kuimarisha matumizi ya vyombo vya habari na majukwaa ya kidijitali katika kuwafikia vijana na kuwapatia taarifa kuhusu fursa na programu mbalimbali za maendeleo.
Mhe. Nanauka amesema matumizi bora ya vyombo vya habari ni muhimu katika kuhakikisha taarifa zinawafikia vijana kwa wakati, kuwaongezea uelewa na kuwawezesha kutambua na kutumia fursa zilizopo. Aidha, ameeleza majukumu ya msingi ya Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, kwa lengo la kuwajengea wadau uelewa kuhusu majukumu, utendaji na uendeshaji wa Ofisi hiyo katika kusimamia na kuchochea maendeleo ya vijana.
Amesema ushirikiano thabiti kati ya Ofisi hiyo na vyombo vya habari ni muhimu katika kuongeza wigo wa kuwafikia vijana, kuwajengea uelewa kuhusu fursa zilizopo na kuwawezesha kuzitumia, huku akisisitiza matumizi ya majukwaa ya kidijitali na njia nyingine za mawasiliano zinazowafikia vijana kwa wakati na kwa ufanisi.
Kwa upande wake, Shafii Mpanja amesema kikao hicho kimekuwa na umuhimu mkubwa kwa kuwa kimewapa wadau nafasi ya kutoa maoni na mapendekezo yatakayosaidia kuwafikia vijana wengi zaidi, ili waweze kutambua na kunufaika na fursa na programu mbalimbali za maendeleo ya vijana.
Kerryn Mbatude ameipongeza Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana kwa kubuni njia mbalimbali za kuwafikia na kuwahudumia vijana, ikiwemo kuanzisha mfumo wa YES, akisema mfumo huo ni mkombozi kwa vijana kwa kuwa unawawezesha kupata taarifa sahihi, kufikia fursa mbalimbali kwa wakati, hivyo kuwafanya kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nana...
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imeitaka Ofisi ya Rais...
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imepongeza maandalizi...
WAZIRI MKUU wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba...
-Asifu bunifu za Vijana zinazozalisha ajira -Atoa ahadi ya kuongeza bajeti ya V...