Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nanauka, amesema kuwa Serikali imeboresha mifumo ya mawasiliano ili kuwapa vijana nafasi ya kueleza changamoto zao na kupata majibu na utatuzi kwa wakati, kupitia Kituo cha Mawasiliano, Mfumo wa YES na Jukwaa la Vijana (Vijana Platform).
Akizungumza katika kipindi cha Good Morning cha Wasafi FM, Mhe. Nanauka amesema kuwa taarifa zinazowasilishwa na vijana kupitia mifumo hiyo zinaiwezesha Serikali kuelewa changamoto na mahitaji halisi ya vijana katika maeneo mbalimbali na hivyo kupanga programu zinazolenga kutatua changamoto hizo.
Katika eneo la elimu na ujuzi, Mhe. Nanauka amesema Serikali inalenga kuhakikisha kuwa mafunzo yanayotolewa yanaendana na mahitaji ya soko la ajira na viwanda, kupitia ushirikiano na taasisi za elimu, zikiwemo VETA na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU). “Sasa hivi tunachotaka ni kuwa, elimu inayotolewa ilingane na mahitaji ya mazingira husika,” amesema.
Aidha, kuhusu malezi na makuzi ya vijana, Mhe. Nanauka amesisitiza umuhimu wa familia kushiriki moja kwa moja katika malezi, akisema jukumu la kujenga vijana wenye uwezo wa kukabiliana na misukosuko ya maisha na kudhibiti hisia haliwezi kuachwa kwa Serikali pekee. “Taifa haliwezi kulelewa na Serikali peke yake, malezi yanaanzia ngazi ya familia,” ameongeza
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nana...
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imeitaka Ofisi ya Rais...
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imepongeza maandalizi...
WAZIRI MKUU wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba...
-Asifu bunifu za Vijana zinazozalisha ajira -Atoa ahadi ya kuongeza bajeti ya V...