Ofisi ya Rais
Maendeleo ya Vijana
UWANJA WA NDUA, MAMBO SAFI KWA UZINDUZI WIKI YA VI...

UWANJA WA NDUA, MAMBO SAFI KWA UZINDUZI WIKI YA VIJANA.

10 Oct, 2026
UWANJA WA NDUA, MAMBO SAFI KWA UZINDUZI WIKI YA VIJANA.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana Bi.Jenifa Christian Omolo na Katibu Mkuu Wizara ya Kazi,Ajira,Vijana na Uwezeshaji Bi.Salama Mbarouk  Khatib wameridhishwa na maandalizi yanayoendelea kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Ndua vitakavyotumika katika uzinduzi wa wiki ya Vijana Kitaifa,2026

Makatibu Wakuu hao wamepokea taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi Dkt.Mollel Meigalu kuwa tayari wiki ya Vijana imeanza tangu tarehe 8 Oktoba,2026 na Vijana washiriki,Wananchi toka ndani na nje ya nchi wameonesha mwitikio mkubwa.

Kwa upande Mkurugenzi Suleiman Mvunye, mwenye dhamani ya Uratibu wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa amesema Mwenge wa Uhuru utaingia Mkoani Rukwa tarehe 10 Oktoba,2026 na baada ya kukimbizwa kwenye Halmashauri zake 4, tarehe 14 utafikia Kilele huku maandalizi ya shughuli za kilele yakiwa yamekamikika

Aidha,baada ya kupokea taarifa hiyo Makatibu Wakuu hao walipata fursa ya kutembelea Mabanda kuona huduma likiwemo Banda ya Mwl.Nyerere foundation,Rais Karume pamoja na Vijana Wabunifu walikuja na teknolojia rafiki kwa mazingira ya Tanzania.

Wiki ya Vijana Kitaifa,2026 inazinduliwa rasmi tarehe 10 Oktoba,2026 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Mwigulu Lameck Nchemba