SERIKALI kupitia Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana imeendelea kuchukua hatua madhubuti za kuleta mapinduzi ya kiuchumi na kijamii kwa vijana. Katika kuonyesha dhati ya hilo, Katibu Mkuu, Bi. Jenifa Christian Omolo, amekutana na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini Tanzania, Bi. Susan Ngongi Namondo, kujadili maeneo makuu ya ushirikiano yatakayobadilisha maisha ya kizazi cha sasa na kijacho.
Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 30 Septemba 2026, katika Ofisi za Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma. Katibu Mkuu, Bi. Omolo ameelezea ajenda nzito zinazogusa moja kwa moja changamoto za ajira, fursa za kiuchumi, afya ya akili, na ushiriki wa vijana katika maamuzi ya kitaifa na kimataifa.

Hata hivyo, wajumbe wote wamejadili mambo manne ya msingi, ikiwa ni Pamoja na Uanzishwaji wa Baraza la Vijana na maboresho ya Sheria, Afya ya Akili na Makundi Maalumu, ushiriki katika Jukwaa la Vijana la Umoja wa Mataifa (ECOSOC) mwaka 2027 na Uchumi wa Kidijitali na Sekta Binafsi ikiwa ni utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Kufuatia mazungumzo hayo, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana imepokea na kuendelea kusimamia utekelezaji wa maazimio saba ya haraka, ikiwemo kuratibu kikao cha pamoja na wakuu wa mashirika ya UN yaani (UNDP, UNCDF na UNICEF), kuwasilisha Mfumo wa Uratibu wa Maendeleo ya Vijana, na kuharakisha matokeo ya utafiti wa vijana uliofanywa kwa ushirikiano na Chuo Kikuu Mzumbe.
Sanjari na hayo, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini Tanzania, Bi. Susan Ngongi Namondo amesema "Vijana ndio nguzo kuu ya taifa. Tunahitaji kuona rasilimali na mipango ikiwanufaisha moja kwa moja vijana walioko vijijini, mijini, na hata wale walio katika mazingira magumu."
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nana...
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imeitaka Ofisi ya Rais...
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imepongeza maandalizi...
WAZIRI MKUU wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba...
-Asifu bunifu za Vijana zinazozalisha ajira -Atoa ahadi ya kuongeza bajeti ya V...