SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka mkazo katika kupima matokeo ya fursa na uwezeshaji unaotolewa kwa vijana ili kuhakikisha kuwa majukwaa ya majadiliano yanazaa manufaa yanayoonekana na kupimika.
Akifungua Kongamano ya Vijana Kitaifa 2026 linaloendelea Manispaa ya Sumbawanga, mkoani Rukwa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nanauka amesema ya kuwa majukwaa ya vijana yanapaswa kuzingatia matokeo yanayopimika badala ya kuishia katika mijadala isiyoleta mabadiliko.

“Tunatamani majukwaa haya yawe na matokeo yanayopimika. Kwamba leo tunapokutana hapa Sumbawanga, baada ya miezi mitatu au minne, tutajipima namna gani kwa fursa ambazo zimetolewa hapa au uwezeshaji ambao umefanyika,” amesema Waziri Nanauka.
Amesema kuwa, Serikali inalenga kuelekeza muda na rasilimali zaidi katika utekelezaji wa maazimio na ufuatiliaji wa matokeo, huku wataalamu wakiwa na jukumu la kusimamia utekelezaji huo kwa kutumia vipimo vitakavyowezesha kutathmini manufaa ya fursa zinazotolewa kwa vijana.
Katika kuimarisha upatikanaji wa taarifa za fursa, Waziri Nanauka amesema Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana imeanzisha Mfumo wa Youth Empowerment System (YES), kufuatia maoni ya vijana kuhusu kuchelewa kwa taarifa na changamoto za usawa katika upatikanaji wa fursa. Kupitia mfumo huo, vijana wanaweza kuweka sawa taarifa za elimu na ujuzi wao pamoja na kuainisha mahitaji yao, yakiwemo ufadhili wa masomo, mitaji na mafunzo ya kuongeza ujuzi, ili kupata taarifa za fursa zinazolingana na mahitaji yao kupitia simu za mkononi.

Akichangia katika kongamano hilo, Bi. Elizabeth Florence Mtepa amewahimiza vijana wenzake kujisajili kwenye Mfumo wa YES ili kupata taarifa sahihi kuhusu fursa katika sekta mbalimbali, zikiwemo kilimo na ufugaji. Amesisitiza umuhimu wa vijana kutumia mfumo huo kufuatilia fursa zinazoweza kuwasaidia kujikwamua kiuchumi na kuleta maendeleo kwa taifa.
Naye Imani James Joram amewataka vijana kuchangamkia fursa zinazotolewa na Serikali na kutumia kikamilifu zile zinazopatikana katika maeneo yao ili kuanzisha na kukuza shughuli za uzalishaji na ujasiriamali.
Aidha Wiki ya Vijana Kitaifa 2026 inafanyika kuanzia Oktoba 8 - 14 Oktaba, katika Manispaa ya Sumbawanga, mkoani Rukwa, ikiwa na kaulimbiu isemayo “Mazingira Tofauti, Fursa Sawa kwa Vijana.”
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nana...
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imeitaka Ofisi ya Rais...
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imepongeza maandalizi...
WAZIRI MKUU wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba...
-Asifu bunifu za Vijana zinazozalisha ajira -Atoa ahadi ya kuongeza bajeti ya V...