Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amezitaka nchi za Afrika na mataifa ya Ghuba kuweka haki na usalama wa wafanyakazi wahamiaji kuwa kipaumbele katika utekelezaji wa mifumo ya uhamaji wa nguvu kazi.
Dkt. Mwinyi amesema hayo leo, Oktoba 6, 2026, jijini Dar es Salaam wakati akifungua Majadiliano ya Pili ya Doha kuhusu Uhamaji wa Nguvu Kazi (Doha Dialogue II), ambayo wamewakutanisha viongozi na wawakilishi kutoka Afrika, Umoja wa Afrika (AU), nchi za Ghuba (GCC+), mashirika ya kimataifa, waajiri na wafanyakazi kujadili namna ya kuimarisha uhamaji salama na wenye haki wa nguvu kazi.
Amesema mfanyakazi anayekwenda kufanya kazi nje ya nchi anapaswa kupata taarifa sahihi kabla ya kuondoka, ikiwamo kuhusu ajira, mkataba, mshahara na mazingira ya kazi, huku akisisitiza mchakato wa kuajiri kuwa wa wazi, wa haki na unaozingatia viwango vya kazi.
“Uhamaji wa nguvu kazi si suala la kuvuka mipaka pekee, bali linahusu maisha na riziki za familia, waajiri pamoja na uchumi wa nchi.”
Amesema wafanyakazi wahamiaji bado wanakabiliwa na changamoto kama gharama kubwa za uajiri, kunyimwa taarifa muhimu, kutolipwa au kucheleweshwa mishahara, mazingira yasiyo salama ya kazi na upatikanaji mdogo wa haki, hivyo ushirikiano wa nchi zinazotuma na kupokea wafanyakazi ni muhimu katika kukabiliana na changamoto hizo.
Amesisitiza kuwa Majadiliano ya Doha II yanapaswa kuleta hatua za utekelezaji badala ya kubaki kwenye ahadi na matamko, ikiwamo kuimarisha mifumo ya uajiri, utambuzi wa ujuzi, ulinzi wa mishahara na mifumo ya kijamii ili kuhakikisha haki na usalama wa wafanyakazi wahamiaji vinapewa kipaumbele.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nana...
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imeitaka Ofisi ya Rais...
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imepongeza maandalizi...
WAZIRI MKUU wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba...
-Asifu bunifu za Vijana zinazozalisha ajira -Atoa ahadi ya kuongeza bajeti ya V...