Ofisi ya Rais
Maendeleo ya Vijana
WAZIRI NANAUKA AONGOZA HAFLA YA KUKABIDHI GUTA, PI...

WAZIRI NANAUKA AONGOZA HAFLA YA KUKABIDHI GUTA, PIKIPIKI NA BAJAJI KWA VIJANA MTWARA

16 Sep, 2026
WAZIRI NANAUKA AONGOZA HAFLA YA KUKABIDHI GUTA, PIKIPIKI NA BAJAJI KWA VIJANA MTWARA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nanauka, akiongoza hafla ya kukabidhi guta, pikipiki na bajaji kwa vijana wa Mkoa wa Mtwara, kupitia mikopo inayotolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.

Mpango huo ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuwawezesha vijana kupata mitaji na vitendea kazi vitakavyowawezesha kujiajiri, kuanzisha na kukuza shughuli zao za kiuchumi, pamoja na kuongeza fursa za ajira na kipato.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Nanauka amesisitiza umuhimu wa vijana kutumia fursa zinazotolewa na Serikali kwa kuwekeza katika shughuli zenye tija, ili kukuza uchumi wao binafsi, familia na jamii kwa ujumla.

Uwezeshaji huo pia unaendelea kuimarisha utekelezaji wa programu za Serikali zinazolenga kuongeza ushiriki wa vijana katika shughuli za kiuchumi na kuwawezesha kuwa sehemu muhimu ya ujenzi wa uchumi wa Taifa.

Hafla hiyo imekuwa sehemu ya juhudi za Serikali za kuendelea kuwafikia vijana katika maeneo mbalimbali nchini, kuwasikiliza, kutambua changamoto zao na kuwaunganisha na fursa za uwezeshaji zinazolenga kuboresha maisha yao na kuongeza mchango wao katika maendeleo ya Taifa.