Wizara ya Maendeleo ya Vijana Tanzania Bara kwa kushirikiana na Wizara inayoshughulikia masuala ya Vijana Zanzibar, wanatarajia kwa pamoja kuzindua Mwenge wa Uhuru Kitaifa katika Uwanja wa Gombani, Zanzibar, tarehe 02 Aprili 2026.
Tukio hilo linatarajiwa kukutanisha viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na wananchi kwa lengo la kuadhimisha na kuendeleza mila ya mbio za Mwenge wa Uhuru ambazo zimekuwa chachu ya kuhamasisha maendeleo, uzalendo na mshikamano wa Watanzania